top of page
Search

NASAHA - SIKIZA

  • Writer: Unity Radio254
    Unity Radio254
  • Jul 25, 2022
  • 2 min read

Daima nimekuwa mtu wa kudakia tu mambo,sitaki kujua yalianzia wapi,na ni vipi mpaka yakafikia yalipo,nilitaka kuja na suluhisho mwisho wa siku pasi kujua tatizo halisi lilikuwa lipi na jinsi gani linaweza kutatuliwa. Matatizo yapo ya aina tofauti tofauti,na mbinu za kuzisuluhisha ni tofauti pia,suala moja laweza kutatulika kwa njia mia moja ila chaguo lako litategemea na jinsi suala hili lilivyojijenga na mwisho wa siku yatakayotokea baada ya kuchagua kitu fulani.Hapo ndipo niligundua umuhimu wa kusikiliza. Sikiza uelewe yaliyopo,sikiza ujue ni hatua zipi wastahili kuchukua,skiza ili mwisho wa siku usiishie kujutia misimamo yako uliyodhania sawa kumbe yana madhara, skiza upate maarifa,kwani ni muhimu kuliko uamuzi. Usisikilize kwa masikio tu,skiza na mtima pia,angalia mambo kwa jicho la tatu,skiliza hata yasiyosemwa kwani ndiyo muhimu zaidi kuliko yanayosemwa wazi wazi,ujumbe unaokanyagiwa ndio wa maana zaidi,alimradi wataka kuzuia majuto,utalazimika kuskiza hata hilo lisilosemeka… Mja afikiapo daraja hii maishani basi twaweza mvika taji la mshauri au hakimu bora. Iwapo umefikia hapa,utagundua kuwa mambo yako yanakuendea sawa,maamuzi yako yanakuwa yenye kukufaidi kwani yamekomaa kutosha.Hata hivyo kuifikia daraja hii sio mchezo,wengine wamejifunza kwa kupitia makali yasioelezeka,wenye busara walitizama tu na wakajifunza,kadhaa walo vichwa maji “siwezi amini mpaka nishuhudie mwenyewe” wamekipata pata pia,kwa raha zao. Hili ni daraja linalotaka subra,mja ni ajitume,awe makini na awe mkweli katika barabara hii kwani ni nyembamba sana,kosa dogo tu unazama,kujinasua nako ni goma lingine tu usilotamani kucheza. Unavyoona mambo wewe sivyo ninavyoyaona mimi,chaweza kuwa sawa kwangu ila laana kwa mwengine. Binadamu ni tofauti,mienendo yao pia,kila mtu amelelewa katika mazingara yanayotofautiana,tuna dini tofauti,mila tofauti na vingine vingi tu ambavyo kila mja ana uhalisia kivyake,licha ya yote haya,sote ni binadamu,sote ni walimwengu,kila mmoja wetu anatafuta njia ya kulisukuma jahazi lake ipasavyo,sote tumo ndani ya sayari hii inayojiita Dunia,hapana bora na aso bora,usahihi wetu huja kutokana na tunavyoona vitu,kila mtu yuko sawa kwenye mtazamo wake,na itahitaji subra kumkosoa iwapo mtazamo wake unapingana na sheria za kibinadamu. Mwenzenu nipo najitahidi nikitumai nitavuna vya thamani kesho ikija.

Rehema Ravoga

 
 
 

Recent Posts

See All
BEEPING KPLC TOKENS

This week, KPLC was the top gainer in the NSE rising by 23.13%. It’s also up 15% YTD. Did Ndindi Nyoro finally convince Kenyan...

 
 
 
SETTING UP A FINANCIAL LIFE

Many people don’t know how to set up their finances. Here’s a step by step guide on how to set up your financial life. We will cover: ...

 
 
 

Comments


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

+254 798649289

  • Facebook
  • Twitter
  • Instagram

©2022 by Unity Radio 254. Proudly created with Wix.com

bottom of page